LINDA Party Yaenda Mahakamani Kupinga Matumizi ya Jina “Linda Mwananchi”

Share this story

Wamiliki wa LINDA Party wamewasilisha kesi mahakamani kupinga matumizi ya jina “Linda Mwananchi”, wakidai kuwa walianza mchakato wa kusajili jina hilo tangu mwaka 2024.

Wamesema matumizi ya jina hilo yanaweza kusababisha mkanganyiko kwa wananchi, hasa kutokana na LINDA Party kuwa na uungwaji mkono katika maeneo mbalimbali nchini.

Hatua hiyo imekuja saa chache baada ya kundi linaloongozwa na Sifuna kupinga uamuzi wa kuzuia ombi lao la kusajili Linda Mwananchi kama chama cha kisiasa.

Mzozo huo sasa unatarajiwa kusikilizwa na Political Parties Disputes Tribunal, ambayo itaanza kushughulikia kesi iliyowasilishwa na upande unaoongozwa na Sifuna dhidi ya uamuzi wa kuzuia usajili wa Linda Mwananchi kama chama cha kisiasa.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post “See you at the altar, my love.” – Isaya Yunge