Mucho Mangoes Yachaguliwa Kwenye Mpango wa Biashara kati ya Kenya na Ujerumani

Kampuni ya Kenya ya Mucho Mangoes Ltd imechaguliwa miongoni mwa kampuni 21 za nchini zitakazoshiriki katika mpango wa Partnering in Business with Germany, unaolenga kuimarisha ushirikiano wa kibiashara kati ya kampuni za Kenya na Ujerumani.
Mpango huo unatekelezwa na GIZ kwa niaba ya Wizara ya Shirikisho ya Ujerumani inayosimamia Masuala ya Uchumi na Nishati, na kuendeshwa kupitia AHP International pamoja na German Business Development Centre (BDC).
Lengo kuu la mpango huo ni kuziandaa kampuni za Kenya zilizo tayari kwa masoko ya kimataifa ili kujenga ushirikiano wa muda mrefu wa kibiashara na kampuni kutoka Ujerumani, hasa katika masuala ya biashara na uuzaji wa bidhaa katika masoko ya kimataifa.

Afisa Mkuu Mtendaji (CEO) wa Mucho Mangoes, Didas Mzirai, alihudhuria hafla ya kuwaaga washiriki iliyofanyika Nairobi Ijumaa, Septemba 25, ambapo hafla hiyo iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, State Department for Industry, Dkt. Juma Mukhwana, pamoja na maafisa kutoka Ubalozi wa Ujerumani jijini Nairobi.
Kwa sasa, CEO wa Mucho Mangoes yuko Mannheim, Ujerumani, akishiriki katika shughuli mbalimbali za mpango huo kwa lengo la kukuza ujuzi wa biashara, kufungua fursa za masoko ya kimataifa na kujenga uhusiano na washirika wa kibiashara nchini Ujerumani.
Ushiriki wa Mucho Mangoes katika mpango huo unaweka kampuni hiyo miongoni mwa wafanyabiashara wa Kenya wanaolenga kupanua shughuli zao na kufikia masoko ya kimataifa kupitia ushirikiano wa kibiashara


