Bruno Fernandes ametwaa tuzo mbili za PFA!
Kiungo na nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, ameshinda tuzo ya PFA Players’ Player of the Year, baada ya kutambuliwa kwa kiwango chake bora msimu uliopita.
Tuzo hiyo hutolewa na Professional Footballers’ Association (PFA) na hupigiwa kura na wachezaji wenza wa soka nchini England.
Ushindi huo unaongeza heshima kwa Fernandes, ambaye amekuwa mmoja wa wachezaji muhimu zaidi wa Manchester United katika misimu ya hivi karibuni.
Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA — Players’ Player of the Year
Amechaguliwa kwenye Kikosi Bora cha Mwaka cha PFA — PFA Team of the Year
