“See you at the altar, my love.” – Isaya Yunge

Share this story

Mfanyabiashara wa teknolojia kutoka Tanzania, Isaya Yunge, amezua gumzo miongoni mwa mashabiki baada ya kushiriki ujumbe wa kimapenzi kwa Charlene Ruto, akidokeza kuhusu hatua inayofuata katika safari yao ya mapenzi.

Yunge alichapisha video ya kimapenzi akiwa pamoja na Charlene, akiambatanisha ujumbe uliolenga imani, mapenzi na kumtumainia Mungu katika mipango ya maisha yao.

Ujumbe wake ulihitimishwa kwa maneno:

“See you at the altar, my love.” 💍❤️

Pia aliambatanisha emoji za bibi na bwana harusi pamoja na pete, huku akitumia hashtag #CAndI na #SaveTheDate, jambo lililowafanya mashabiki wao kuanza kutazamia kwa hamu ndoa yao.

Ujumbe huo umefika siku chache baada ya Charlene Ruto na Isaya Yunge kusherehekea sherehe yao ya kimila ya Koito mnamo Agosti 8, 2026, katika Intonna Heritage Farm, Kilgoris, Kaunti ya Narok, ambapo familia zao zilikutana kusherehekea hatua muhimu katika uhusiano wao.

Ingawa Yunge hakutangaza tarehe rasmi ya harusi, ujumbe wake wa kimapenzi umeongeza msisimko miongoni mwa mashabiki wanaosubiri kuona lini wawili hao watafunga ndoa.

Safari ya Charlene na Yunge inaendelea kuvutia hisia za wengi, huku wawili hao wakisherehekea mapenzi, familia na mila zilizowaleta pamoja.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Watu Saba Wafariki Baada ya Ndege Kuanguka Samburu East