Kariakoo ya Maua Sama Yaondolewa Youtube
Wimbo mpya wa Maua Sama uitwao ‘Kariakoo’, aliouachia hivi karibuni kwa kushirikiana na Ibraah_tz, Jaivah, na GnakoWaraWara, umekumbwa na changamoto baada ya kuondolewa kwenye mtandao wa YouTube kufuatia malalamiko ya ukiukwaji wa hakimiliki. Wimbo huo, ambao ulitolewa Jumatano, ulikuwa umeanza kupata umaarufu kwa kasi na kufanikiwa kuingia katika orodha ya nyimbo zinazotrend, ukichukua nafasi za juu ndani ya masaa 24 ya kwanza.
Kwa mujibu wa Meneja wa Maua Sama, tayari mhusika aliyeripoti hakimiliki ameweza kupatikana, na juhudi za kurejesha wimbo huo zimeshaanza. Mack alifafanua kuwa kuondolewa kwa wimbo huo hakuhusiani na lebo ya WCB_Wasafi, ambapo Lavalava, msanii wa WCB, pia kuachia wimbo wenye jina #Kariakoo siku hiyohiyo.