Hakuna cha Vikapu ni Mziki na Harusi! B Classic 006 na Cate Mpaka Mwisho
Msanii anayekuja kwa kasi katika tasnia ya muziki, B Classic 006, rasmi ameaga maisha ya ubachela baada ya kufunga ndoa leo tarehe 23 Aprili 2026 nyumbani kwao Taveta.
Tukio hilo la kipekee limehudhuriwa na ndugu, jamaa na marafiki wa karibu, likiwa limejaa furaha, shamrashamra na baraka nyingi kwa wanandoa hao wapya. Habari za ndoa hiyo zimepokelewa kwa shangwe na mashabiki wake mitandaoni, wengi wakimpongeza kwa hatua hiyo muhimu ya maisha.
B Classic 006, ambaye amekuwa akijizolea umaarufu kupitia kazi zake za muziki, sasa ameanza ukurasa mpya wa maisha ya ndoa.
Kwa sasa ni rasmi kusema kuwa B Classic 006 “ametoka sokoni,” huku mashabiki wakimtakia kila la heri katika safari yake mpya ya ndoa.
PICHA ZAIDI






