Watu Saba Wafariki Baada ya Ndege Kuanguka Samburu East

Share this story

Watu saba, akiwemo rubani, wamefariki dunia baada ya ndege ndogo kuanguka katika eneo la Sabache Hills, Samburu East.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, ndege hiyo iliyotambuliwa kwa jina Lady Lorry, ilianguka majira ya saa 3:13 asubuhi, ikiwa njiani kutoka Suyian, Laikipia, kuelekea Loisaba Conservancy.

Waliofariki wametajwa kuwa Josh Outran, Roger Duarte, Adam Navaty, Stephen Vascanknez, Henry Parra, Michael Contugi na Suian Suarez.

Ndege hiyo iliharibika vibaya na kushika moto baada ya kuanguka.

Maafisa wa usalama pamoja na timu za uokoaji wanaendelea na shughuli za kuondoa miili na uchunguzi wa chanzo cha ajali, huku mamlaka zikikusanya taarifa zaidi kuhusu kilichosababisha ndege hiyo kuanguka.

🕊️ Pole kwa familia, ndugu na marafiki wa wote waliopoteza maisha katika ajali hiyo.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Omar Artan Aweka Historia, Aitwa na UEFA kwa Mafunzo ya Waamuzi