Kwa Kina Zuchu Kunavuja

Share this story

Mwanamuziki wa Bongo Fleva Zuchu ametangaza rasmi kuwa yeye na aliyekuwa mume wake, Diamond Platnumz, wameachana na kwa sasa wanaendelea na mchakato wa talaka, baada ya kudumu pamoja kwa takribani miaka sita.

Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram leo Jumapili, Zuchu alisema kwa sasa anajikita katika kuponya hisia zake pamoja na kuimarisha afya na kazi zake za muziki.

“Hello my GPG, mimi na aliyekuwa mwenzangu we are now separated and going through a divorce. As for me, muda huu ni wa kupona na kufocus zaidi kwenye afya na kazi zangu. Riziki imeisha, Alhamdulillah. Tulijaribu lakini Allah ana mipango yake na sina budi kuikubali,” aliandika Zuchu.

Tangazo hilo linakuja miezi kadhaa baada ya Zuchu kuthibitisha hadharani, mwezi Juni 2025, kuwa yeye na Diamond walikuwa wamefunga ndoa kwa siri. Kauli hiyo ilitolewa kufuatia tetesi zilizokuwa zikisambaa kwamba Diamond alikuwa amempa talaka tatu.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kutangaza kuachana. Katika miaka ya nyuma, Diamond na Zuchu waliwahi kutangaza kuvunja uhusiano wao mara kadhaa kabla ya kurejeana, jambo lililowafanya mashabiki wengi kuendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa penzi lao.

Kwa sasa, Diamond Platnumz bado hajatoa tamko rasmi kuhusu taarifa hiyo.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Arsenal Yaongeza Kasi Kumnasa Julián Álvarez Kabla ya Pre-Season
Next post Junior Starlets Watinga Kombe la Dunia Baada ya Kuifunga Afrika Kusini kwa Kishindo