TID Afunguka Kuhusu Mahusiano Yake na Wema Sepetu
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva TID amefunguka kuhusu uhusiano wake wa zamani na Wema Sepetu, akidai kuwa ni Wema aliyekuwa wa kwanza kuonyesha hisia zake kwake.
TID amesema licha ya kuwa walikuwa kwenye mahusiano kwa kipindi fulani, mambo yalibadilika baadaye baada ya Wema kumweleza kuwa hampendi tena.
“Nilikuwa kwenye mahusiano na Wema Sepetu, lakini ukweli ni kwamba si mimi niliyetaka kuanza naye, yeye ndiye alinifuata. Baadaye ilifika kipindi akaniambia hanitaki tena,” alisema TID.
Msanii huyo ameongeza kuwa tangu kuachana kwao amekuwa kwenye mahusiano tofauti na wanawake wengine na kwa sasa hana mpango wa kurudiana na mrembo huyo wa zamani.
“Tangu kipindi hicho nimekuwa na wasichana wengi. Ikitokea Wema anataka kurudi, hakuna nafasi tena,” aliongeza.