Hofu Kivuko Cha Likoni Baada Ya Mwanaume Mmoja Kukamatwa Akiwa Na Kitu Kilichoonekana Kama Bunduki

Share this story

Hofu iliongezeka katika Kivuko cha Likoni, Mombasa, baada ya mwanamume mmojai kukamatwa akiwa amebeba kitu kilichoonekana kama bunduki, hali iliyowafanya maafisa wa usalama kuchukua hatua za haraka.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, maafisa walionekana wakimzunguka mwanamume huyo, aliyekuwa amevaa magunia na nguo chakavu, na kumfanyia upekuzi wa kina, jambo lililozua wasiwasi miongoni mwa wananchi kuhusu usalama.

Hata hivyo, akizungumzia tukio hilo, Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi, Gilbert Masengeli, alifafanua kuwa mwanamume huyo hakuwa na bunduki halisi bali ya kuchezea. Kulingana na Masengeli, mtu huyo alibainika kuwa na matatizo ya akili na alipelekwa hospitalini kwa uchunguzi wa kitabibu.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Serikali yapiga hatua kuhalalisha mnazi, kuwapa afueni wakulima wa minazi wa Pwani
Next post ODM Aspirants Reject Zoning Push as Internal Dissent Grows Amid UDA Pressure