Paraguay Yazizima Sherehe Baada ya Kuitoa Ujerumani Kombe la Dunia
Rais wa Paraguay ametangaza leo kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa baada ya timu ya taifa ya nchi hiyo kuisukuma nje Ujerumani kwenye Kombe la Dunia katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo.
Paraguay iliibuka na ushindi mkubwa baada ya drama ya mikwaju ya penalti, jambo lililozua shamrashamra kubwa nchi nzima huku mashabiki wakimiminika mitaani kusherehekea mafanikio hayo ya kihistoria.
Taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini humo zinaeleza kuwa baadhi ya mabaa yalimaliza kabisa bia kutokana na wingi wa watu waliokuwa wakisherehekea ushindi huo usiku kucha.
Mashabiki wa Paraguay wameonekana wakicheza, kuimba na kupiga honi mitaani kana kwamba tayari wamebeba Kombe la Dunia, hali inayoonyesha namna ushindi huo ulivyogusa hisia za wananchi.
Kweli soka lina ladha yake ya kipekee.