“Bubista” Aipa Onyo Argentina Kabla ya Mchezo wa Mtoano

Share this story

Kocha wa timu ya taifa ya Cape Verde, Pedro Leitao Brito maarufu kama “Bubista”, amesema licha ya kuipa heshima Argentina, hawana hofu yoyote kuelekea mchezo wao wa hatua ya 32 bora.

Bubista amesema katika hatua ya mtoano lolote linaweza kutokea, huku akisisitiza kuwa Cape Verde wanaamini zaidi uwezo wao uwanjani kuliko historia au rekodi za wapinzani wao.

Kocha huyo ambaye ameivutia dunia kwa mbinu zake za kimkakati mpaka sasa hajapoteza mchezo hata mmoja kwenye hatua ya makundi, na aliwashangaza wengi baada ya kuizuia Hispania ya Lamine Yamal kushindwa kupata ushindi dhidi yao.

Kwa mujibu wa Bubista, Cape Verde itaingia uwanjani kupambana bila woga wowote, huku akionya kuwa Argentina haitakiwi kuwachukulia kirahisi kwani timu yake inaishi falsafa ya mapambano na nidhamu kubwa ya kiuchezaji.

Mashabiki wengi tayari wanausubiri kwa hamu mchezo huo mkubwa huku Lionel Messi na Argentina wakitarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa Cape Verde inayotajwa kuwa moja ya timu zilizofanya vizuri zaidi kwenye mashindano haya hadi sasa.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post President Ruto set to commission the Ngong Road Flyover
Next post Petition Filed in High Court to Stop NTSA Mandatory Vehicle Inspection