Mashabiki Zaidi ya Milioni 30 Wataka Mbappé Aondoke Real Madrid

Share this story

Nyota wa soka duniani, Kylian Mbappé, amejikuta kwenye presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa Real Madrid baada ya zaidi ya mashabiki milioni 30 kusaini ombi la kutaka aondoke ndani ya klabu hiyo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa kushindwa kuisaidia timu kupata matokeo mazuri pamoja na mwenendo wake nje ya uwanja.

Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa mitandaoni, ombi hilo lilianzishwa siku mbili zilizopita likiwa na lengo la kukusanya saini 200 pekee kutoka kwa mashabiki waliokuwa hawajaridhishwa na kiwango chake. Hata hivyo, ndani ya saa 24 pekee, zaidi ya saini milioni 18 zilikuwa tayari zimekusanywa, huku idadi hiyo ikipanda hadi milioni 30 baada ya saa 48 kupita.

Mashabiki wengi wameonyesha kutoridhishwa na mchango wa Mbappé tangu alipojiunga na Real Madrid mwezi Juni mwaka 2024 akitokea klabu ya Paris Saint-Germain kwa mkataba wa muda mrefu unaotarajiwa kumuweka Santiago Bernabéu hadi mwaka 2029.

Ripoti mbalimbali pia zinadai kuwa baadhi ya wachezaji ndani ya kikosi hicho wamekuwa wakimwona Mbappé kama “msaliti,” hali inayodaiwa kuleta mgawanyiko ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo na kuathiri mshikamano wa timu hiyo yenye mafanikio makubwa barani Ulaya.

Licha ya kuwa mmoja wa wachezaji wenye majina makubwa duniani, Mbappé ameendelea kukosolewa na sehemu ya mashabiki wanaoamini kuwa uwepo wake haujaleta mabadiliko makubwa waliokuwa wakiyatarajia ndani ya kikosi hicho.

Hata hivyo, hadi sasa uongozi wa Real Madrid haujatoa kauli rasmi kuhusu taarifa hizo wala kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Governor Kang’ata Announces He Will Quit UDA