KUHAMISHWA AFCON 2027 HAIKUWA MJADALA.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Mhe. Hamis Mwinjuma amesema kuwa, suala la kuhamishwa kwa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027) kutoka Afrika Mashariki kwenda sehemu nyingine halipo.
Amesema hayo baada ya kumaliza kikao na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Samson Adamu kilichofanyika Aprili 23, 2026 Kampala Uganda, ambacho kiliwakutanisha nchi wenyeji wa mashindano hayo ambayo ni Tanzania, Kenya na Uganda.