UDA Yatinga Kwa Kishindo Katika Uchaguzi mdogo Narok, Elgeyo Marakwet na Samburu

Share this story

Chama cha United Democratic Alliance (UDA) kimeibuka na ushindi mkubwa katika chaguzi mbalimbali za ubunge na uwakilishi wa wadi zilizofanyika katika kaunti za Narok, Elgeyo Marakwet na Samburu, huku wagombea wake wakiongoza kwa tofauti kubwa ya kura dhidi ya wapinzani wao.

Katika uchaguzi wa Mbunge wa Emurua Dikirr Constituency, Afisa Msimamizi wa Uchaguzi alimtangaza David Kipsang Keter wa chama cha UDA kuwa mshindi baada ya kupata kura 18,266.

Mpinzani wake wa karibu, Vincent Kibet Rotich wa chama cha DCP, alimaliza wa pili kwa kupata kura 10,760.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi, jumla ya wapiga kura waliosajiliwa katika eneo hilo walikuwa 44,353, huku kura 29,538 zikipigwa, sawa na asilimia 66.6 ya ushiriki wa wapiga kura.

Katika uchaguzi wa mwakilishi wa wadi ya Endo Ward, mgombea wa UDA Festus Korir Kiprop alitangazwa mshindi baada ya kujizolea kura 4,475.

Mpinzani wake Shadrack Kosgei Chelang’a wa chama cha NDP alipata kura 752 pekee.

Kati ya wapiga kura 14,361 waliojiandikisha, kura 5,260 zilipigwa, kiwango kinachowakilisha asilimia 36.59 ya ushiriki wa wapiga kura.

Aidha, katika uchaguzi wa mwakilishi wa wadi ya Porro Ward, mgombea wa UDA Daniel Lolngojine aliibuka mshindi kwa kupata kura 2,328 dhidi ya mpinzani wake Josphat Jumani Leleur wa chama cha KANU aliyepata kura 1,036.

Katika eneo hilo, jumla ya wapiga kura waliosajiliwa walikuwa 6,358 huku kura 4,194 zikipigwa, sawa na asilimia 65.96 ya ushiriki wa wapiga kura.

Matokeo hayo yanaendelea kuonyesha nguvu ya kisiasa ya UDA katika maeneo mbalimbali nchini huku chama hicho kikizidi kuimarisha ushawishi wake kuelekea uchaguzi mkuu ujao.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Ruto and UN Chief Guterres Launch Sh43.8 Billion Nairobi Expansion Project