Ndoa ya Fahyma Na Rayvanny Bado Sana

Share this story

Katika mahojiano ya hivi karibuni, Rayvanny ameweka wazi kuwa suala la ndoa si jambo la kukurupuka. Moja ya sababu kubwa alizozitaja hapo awali ni umri wa Fahyma. Rayvanny alieleza kuwa alitaka kumpa muda mpenzi wake huyo ili akue kiumri na kifikra ili anapoingia kwenye majukumu ya mke, awe amekomaa vya kutosha kuhimili kishindo cha maisha ya ndoa ya mastaa.

Aidha, Rayvanny amesisitiza kuwa anataka kufanya ndoa ya kihistoria. Chui hataki ndoa ya kawaida; anataka sherehe itakayozungumzwa Afrika nzima. Hii inapelekea maandalizi kuchukua muda mrefu zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Inasemekana mazingira ya kazi na ratiba za kimataifa za Rayvanny pia zimekuwa zikiingiliana na mipango hiyo ya kiserikali na kidini.

Kwa upande wake, Fahyma amekuwa akionyesha utulivu wa ajabu. Akihojiwa kuhusu kuchelewa kwa pete ya ndoa (licha ya kupewa pete ya uchumba), mwanamitindo huyo ameeleza kuwa ana amani na mahusiano yake. “Ndoa ni baraka kutoka kwa Mungu, na itafanyika wakati sahihi ukifika. Rayvanny ni baba wa mtoto wangu na mume wangu wa maisha, sioni haja ya kumlazimisha sasa hivi,” alisema Fahyma.

Kauli hii imewashangaza wengi wanaodhani kuwa mrembo huyo anashinikiza ndoa hiyo ifanyike haraka. Fahyma anaonekana kujikita zaidi katika kukuza chapa yake ya urembo na kumlea mtoto wao, Jaydan, huku akimwachia Rayvanny nafasi ya kuandaa “shughuli” hiyo nzito anayoipanga.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Kenya inatimiza wajibu wa CAF kuwa mwenyeji mwandalizi wa AFCON
Next post Godhana aonya juu ya uharibifu wa miundombinu ya maji