Mrembo Vera Sidika Aonesha Sura yake Mpya Baada ya Sajari
Mrimbwende maarufu katika masuala ya urembo nchini Kenya, Vera Sidika ameonyesha sura yake mpya baada ya kufanyiwa upasuaji nchini Uingereza.
Kwa mujibu wa mitandao mbalimbali nchini Kenya, Vera ameonyesha video kwenye ‘Instagram stories’ yake kuhusu ziara yake katika kliniki moja iliyopo nchini Uingereza ambapo alifanyiwa upasuaji huo.
Katika moja ya video alionyesha, cream ya kufa ganzi inayotumika kupaka uso wake kabla ya shughuli nzima ya upasuaji kuanza. Alishiriki picha za kabla na baada ya kufanyiwa upasuaji huo na baada ya upasuaji uso wake ulionekana mwembamba kuliko ulivyokuwa kabla.
Vera alicheka na kusema kwamba hakuwa na taya kabla ya huduma hiyo na ameshukuru kwa kazi iliyofanywa usoni mwake. “Mara yangu ya kwanza kabisa. Unauliza Vera ana sura ngapi? Niko hapa kununua uso. Nina nyuso 135. Sikuwa na mstari wa taya kabla ya upasuaji,” ilieleza video hiyo.
‘Rhytidectomy’ ni aina ya upasuaji wa kivipodozi ambao hufanya uso uonekane mchanga na kuzuia ngozi kulengea. Zaidi ya hayo, unaweza kusaidia kulainisha mikunjo ya ngozi karibu na taya na mashavu.
Jina lingine la upasuaji huo ni ‘rhytidectomy’ ambapo pande la ngozi hutolewa kila upande wa uso wakati wa upasuaji pia ngozi ya ziada huondolewa na tishu zilizo chini ya ngozi hubadilishwa. Matokeo yake ni kwamba uso huonekana wa ujana zaidi. Sura mpya mara kwa mara ni pamoja na kuimarisha mwonekano wa shingo. Kupunguza mafuta ya shingo na ngozi iliyolegea