Junior Starlets Watinga Kombe la Dunia Baada ya Kuifunga Afrika Kusini kwa Kishindo

Timu ya taifa ya wanawake ya Kenya chini ya umri wa miaka 17, Junior Starlets, imefuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA U-17, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo wa marudiano uliochezwa Jumapili, Julai 12, kwenye Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Baada ya ushindi huo, Kenya ilifuzu kwa jumla ya mabao 5-1 katika michezo miwili, ikionyesha ubora mkubwa dhidi ya wapinzani wao.

Junior Starlets walionyesha moyo wa mapambano kwa kufanya comeback ya kuvutia, wakigeuza mchezo na kuhakikisha wanapata ushindi uliowapeleka kwenye fainali za Kombe la Dunia kwa mara nyingine.
Ushindi huo ni mafanikio makubwa kwa soka la wanawake nchini Kenya na unaendeleza safari ya kuvutia ya kikosi hicho, ambacho kimeendelea kuwapa matumaini Wakenya kwa kiwango chake bora katika mashindano ya kimataifa.
