Ronaldo Aizungumzia Mechi Dhidi ya Hispania
Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo, amesema wanafahamu ugumu wa mchezo wao dhidi ya Hispania huku akiitaja timu hiyo kama moja ya zinazopewa nafasi kubwa ya kutwaa Kombe la Dunia.
Ronaldo amesema katika hatua hii ya mashindano hakuna mechi nyepesi kwani kila timu imefika hapo kwa ubora wake.
“Tunajua vizuri jinsi mechi dhidi ya Hispania itakuwa ngumu. Wao ni miongoni mwa timu zinazopigiwa upatu kushinda Kombe la Dunia. Kila mchezo katika hatua hii ni mgumu sawa. Hakuna mchezo mwepesi.”
Nyota huyo wa Ureno ameongeza kuwa kikosi chao kimejiandaa kikamilifu na kinaifahamu vizuri Hispania, hivyo anatarajia mchezo wa ushindani mkubwa.

“Tumejiandaa kikamilifu, na tunamjua vizuri mpinzani wetu. Itakuwa mechi yenye uwiano mkubwa, na mwisho wa siku tutaona mchezo utaleta nini.”
Kauli ya Ronaldo imeongeza hamasa kuelekea pambano hilo kubwa ambalo mashabiki wengi wa soka duniani wanasubiri kwa hamu.