Pape Gueye Atangaza Kupumzika Timu ya Taifa ya Senegal Baada ya Kuondolewa Kombe la Dunia
Kiungo wa Senegal, Pape Gueye, hakuweza kuficha maumivu na hasira zake baada ya timu hiyo kushindwa kufuzu hatua ya 16 bora kwenye Kombe la Dunia 2026.
Gueye ameilaumu benchi la ufundi kwa kile alichokitaja kuwa udhaifu wa kimkakati uliogharimu Senegal nafasi ya kusonga mbele kwenye mashindano hayo makubwa.
Kupitia kauli yake, kiungo huyo amesema:
“Nitarudi baadaye kuzungumzia zaidi kuhusu kuondolewa kwetu… lakini kwa leo natangaza kuwa mradi benchi hili la ufundi litaendelea kuwepo, nitachukua mapumziko kutoka timu ya taifa.”
Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wa Senegal, huku wengi wakitafsiri matamshi yake kama ishara ya mgogoro mkubwa ndani ya kikosi hicho baada ya kutolewa mapema kwenye mashindano.
Pape Gueye ni miongoni mwa wachezaji muhimu wa Senegal na kauli yake inaweza kuongeza presha kwa benchi la ufundi pamoja na viongozi wa soka nchini humo.