Matonya kizimbani kwa madai ya unyanyasaji wa kingono
Msanii wa Tanzania, Sefu Shabani 43, anayejulikana zaidi kama Matonya amekamatwa na kushtakiwa nchini Kenya kwa madai ya unyanyasaji wa kingono
Matonya, ambaye amewahi kutamba na nyimbo maarufu kama ‘Vaileti’ na ‘Anita’, amekanusha tuhuma zote zinazomkabili Mahakamani hapo.
Baada ya kusomewa mashtaka, Mahakama imemruhusu kuwa nje kwa dhamana, huku ikiweka masharti ya kukabidhi hati yake ya kusafiria Mahakamani.
Aidha, Msanii huyo amezuiliwa kusafiri nje ya eneo husika bila kupata kibali rasmi kutoka Mahakama hiyo hadi kesi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.