Mshambuliaji wa Cape Verde Awaacha Mashabiki Wakivutiwa Baada ya Bao dhidi ya Argentina ❤️⚽

Share this story

Mshambuliaji wa Cape Verde aliiba show jana baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Argentina kisha kukimbilia jukwaani kushangilia pamoja na mchumba wake mbele ya mashabiki waliokuwa wamejaa uwanjani.

Tukio hilo liligeuka kuwa moja ya vivutio vikubwa vya mchezo huo, huku picha na video zikisambaa kwa kasi mitandaoni kutokana na namna lilivyogusa hisia za wengi.

Mbali na shangwe hizo za kimapenzi, bao lenyewe lilikuwa la kiwango cha juu sana na tayari linaonwa na wengi kama moja ya mabao bora zaidi kuwahi kufungwa kwenye mashindano hayo.

Kilichoongeza uzito wa bao hilo ni ukweli kwamba lilifungwa dhidi ya golikipa hatari wa Argentina, Emiliano Martinez, anayefahamika kwa uwezo wake mkubwa wa kuokoa mipira migumu na kuwatesa washambuliaji wengi duniani.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Cristiano Ronaldo Akaribia Kuaga Timu ya Taifa ya Ureno Baada ya Miaka 23
Next post Vozinha Aacha Historia Kombe la Dunia Licha ya Cape Verde Kutolewa 🇨🇻🧤🔥