Crystal Palace Yaandika Historia Kwa Kutwaa UEFA Europa Conference League
Crystal Palace imeandika historia mpya baada ya kutwaa ubingwa wa UEFA Europa Conference League kufuatia ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Rayo Vallecano katika fainali iliyochezwa kwenye dimba la Red Bull Arena mjini Leipzig, Ujerumani.
Bao pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 51 kupitia mshambuliaji Jean-Philippe Mateta, aliyewapa Palace ushindi mkubwa na kombe lao la kwanza la Ulaya katika historia ya klabu hiyo.
Ushindi huo pia umeifanya Crystal Palace kuwa timu ya kwanza katika kipindi cha miaka 38 kushinda taji la Ulaya kwenye fainali yake ya kwanza kabisa katika mashindano ya bara Ulaya.

Kocha Oliver Glasner ameondoka klabuni humo kwa heshima kubwa baada ya mchezo huo, huku akiwa ameiongoza Palace kutwaa mataji matatu muhimu ndani ya muda mfupi. Chini ya Glasner, Palace ilitwaa Kombe la FA mwaka 2025, Ngao ya Jamii dhidi ya Liverpool mwaka huo huo, na sasa UEFA Europa Conference League ya 2026.
Mafanikio hayo yanaendelea kuthibitisha ubora wa klabu za London katika mashindano ya Ulaya, ambapo Crystal Palace imekuwa timu ya tatu kutoka England kushinda taji kubwa la Ulaya ndani ya miaka mitano iliyopita, baada ya Chelsea FC na West Ham United.
Matokeo ya Fainali:
Crystal Palace 1-0 Rayo Vallecano
⚽ 51’ Jean-Philippe Mateta