AL-SHABAAB WAUA WANAJESHI 54 RAIA WA UGANDA

Share this story

Takriban wanajeshi 54 wa Uganda akiwemo kamanda mmoja waliuawa na al-shabaab wakati wa shambulizi nchini Somalia wiki moja iliyopita, Rais Yoweri Museveni amethibitisha.

Hii ni baada ya magaidi hao kushambulia kambi ya walinda amani wa Umoja wa Afrika huko Bulamarer, kilomita 130 kusini magharibi mwa Mogadishu.

Museveni katika taarifa yake Jumamosi pia alisema kuwa makamanda wawili ambao ‘walifanya makosa’ wamekamatwa na watakabiliwa na mashtaka katika Mahakama ya Martial.

Wiki iliyopita Museveni alisema kumetokea vifo vya Waganda lakini hakutoa maelezo zaidi kuhusu Wanajeshi hao wanaohudumu katika Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika Nchini Somalia (ATMIS).


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post ZAIDI YA WATU 300 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA TRENI
Next post Tazama jinsi timu ya #yanga ilivyopewa heshima ugenini