Dereva wa boda boda auawa katika eneo la Mwangaza, Taveta na piki piki yake kuibiwa
Dereva mmoja wa boda boda amepatikana ameuawa katika eneo la Mwangaza, Taveta, huku pikipiki yake ikidaiwa kuchukuliwa na watu wasiojulikana.
Mwili wa marehemu ulipatikana asubuhi ya leo ukiwa na dalili zinazoashiria kuwa huenda alifanyiwa mateso kabla ya kuuawa.
Hadi sasa, hakuna taarifa rasmi kutoka kwa vyombo vya usalama kuhusu utambulisho wa washukiwa au sababu kamili ya mauaji hayo.
Hata hivyo, tukio hilo linadaiwa kuhusishwa na mtandao wa wizi wa pikipiki ambao umekuwa ukiripotiwa katika maeneo mbalimbali ya Taveta.
Uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha tukio hilo na kuwafichua waliohusika.