Guinea yaomboleza mashabiki 56 waliokufa katika vurumai za penalti, kadi nyekundu

Share this story

PENALTI tata na kadi mbili nyekundu zilizotolewa na refa zilisababisha vifo 56 kufuatia vurumai zilizozuka wakati wa mechi kati ya Labe na wenyeji Nzerekore, nchini Guinea, Jumapili.

Mechi hiyo ya nuksi ilikuwa fainali ya mashindano yaliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Mamady Doumbya. Rais Doumbya aliingia mamlakani kupitia mapinduzi Septemba 2021.

Katika mchuano huo refa alifanya maamuzi ya kutatanisha yaliyoudhi mashabiki wa Labe na wakaanza kumrushia mawe kwa hasira. Polisi walijaribu kutuliza hali kwa kurusha vitoa machozi upande wa Labe bila mafanikio.

“Fujo zilianza wakati refa alitoa uamuzi wa utata uliofanya mashabiki kuingia uwanjani,” mtu mmoja aliyeshuhudia kisa  hicho aliambia wanahabari.

Mwingine akaongeza kupitia simu: “Mawe yalianza kutupwa kisha polisi wakaingia na kufyatua vitoa machozi kutawanya watu. Katika patashika na vuruumai zilizofuata niliona watu wakianguka chini, wasichana na watoto wakikanyangwa. Lilikuwa tukio bovu sana, la kutisha na kusikitisha.”


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post President Biden issues pardon to son Hunter on gun and tax charges
Next post Wundanyi : Eneo La Paranga Kufaidi Mradi Wa Umeme