Vozinha Aacha Historia Kombe la Dunia Licha ya Cape Verde Kutolewa πŸ‡¨πŸ‡»πŸ§€πŸ”₯

Share this story

Ingawa Cape Verde wameaga mashindano, golikipa wao mkongwe Vozinha ameondoka akiwa mmoja wa mastaa waliotikisa zaidi Kombe la Dunia mwaka huu.

Maonyesho yake bora langoni yamevutia mashabiki wengi duniani na kumletea umaarufu mkubwa sana kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram.

Kabla ya mashindano hayo kuanza, Vozinha alikuwa na takribani wafuasi 50,000 pekee kwenye akaunti yake ya Instagram. Lakini baada ya kuonyesha kiwango cha juu dhidi ya mataifa makubwa duniani, idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia zaidi ya milioni 19. 😳πŸ”₯

Kinachofanya simulizi hilo kuwa la kipekee zaidi ni kwamba nchi yake ya Cape Verde ina jumla ya wananchi wasiopungua laki 4 pekee.

Kwa wengi, Vozinha sio tu ameisaidia Cape Verde kujitangaza duniani, bali ameonyesha kuwa hata mataifa madogo yanaweza kutoa nyota wakubwa kupitia soka. ⚽🌍


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Mshambuliaji wa Cape Verde Awaacha Mashabiki Wakivutiwa Baada ya Bao dhidi ya Argentina ❀️⚽