Dangote Awasili Lamu kwa Uzinduzi wa Mradi wa Kiwanda cha Kusafisha Mafuta
Mfanyabiashara na mwekezaji bilionea kutoka Nigeria, Aliko Dangote, amewasili Lamu kuelekea hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi la mradi wa kiwanda cha kusafisha mafuta cha East African Oil Refinery.
Dangote alipokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Manda, Lamu, na Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kenya Airports Authority (KAA), Moses Wekesa.
Hafla hiyo ya kihistoria inatarajiwa kufanyika kesho na mwenyeji wake akiwa Rais William Ruto, huku ikiashiria hatua muhimu katika utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa sekta ya mafuta nchini Kenya.