Mbappé Aipeleka Ufaransa Robo Fainali kwa Bao Lake la 19 Kombe la Dunia

Share this story

Kylian Mbappé ameendelea kuandika historia kwenye Kombe la Dunia baada ya kufunga bao lake la 19 kwenye michuano hiyo wakati Ufaransa ikiichapa Paraguay mabao 1-0 na kutinga robo fainali.

Bao hilo lilipatikana dakika ya 70 kupitia mkwaju wa penalti uliompa mshambuliaji huyo nafasi ya kufikisha mabao saba kwenye Kombe la Dunia 2026 na kuongoza orodha ya wafungaji bora sambamba na Lionel Messi. ⚽🔥

Kwa ushindi huo, Les Bleus wamefanikiwa kushinda michezo yote mitano waliocheza kwenye mashindano haya kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yao ya Kombe la Dunia.

Ufaransa sasa itakutana na Morocco katika mchezo mkubwa wa robo fainali unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani. 🇲🇦🇫🇷


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Morocco Waandika Historia Mpya Kombe la Dunia 🇲🇦🔥