Gachagua Atishia Kuhamasisha Gen Z Kuingia ofisi za Serikali
Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua ametishia kuwakusanya Gen Z kuingia afisi za serikali kwa madai ya ubaguzi katika utoaji wa hati za utambulisho.
Gachagua alizungumza wakati wa ibada ya kanisa huko Gatundu Kaskazini ambapo alidai kuwa kuna njama ya serikali kuzima juhudi za vijana wanaotafuta vitambulisho, haswa kutoka mikoa ambayo haipendelei serikali ya Kenya Kwanza.
Naibu raisi huyo wa zamani alifichua upinzani utakuwa na mkutano Jumatatu, Aprili 6 ili kupanga njia ya kusonga mbele, na kuapa kufanya maandamano ikiwa mtindo huo utaendelea.
Matamshi yake yalikuja huku kukiwa na ripoti kutoka Huduma Kenya kwamba maelfu ya hati muhimu, ikiwa ni pamoja na vitambulisho, bado hazijachukuliwa katika vituo vingi.