Taifa Stars Yailaza Niger Bao 1-0

Share this story

Timu ya Tanzania, Taifa Stars, imeonyesha ubabe kwa kuichapa nyumbani timu ya Niger bao 1 – 0 katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.

Bao pekee la ugenini la mchezo huo limefungwa na Charles M’mombwa katika dakika ya 60 ya mchezo.

Ushindi huu unaifanya Taifa Stars kupanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi E, nyuma ya Zambia, na kuimarisha matumaini ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.

Mchezo ujao wa Taifa Stars utakuwa nyumbani, wakipambana na Morocco kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa mnamo Novemba 21, 2023.

Morocco haijacheza mchezo wake kutokana na timu ya Taifa ya Eritrea ambapo pia walikuwa kundi E, kujiondoa.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Argentina walipoteza mchezo wao jana dhidi ya Uruguay kwa magoli 2-0.
Next post DIAMOND PLATNUMZ APONGEZA HARMONIZE KUSHINDA TUZO TATU