MITIHANI YA KCPE NA KPSEA IMETAMATIKA.
Mitihani ya kitaifa la darasa la nane na KPSEA imekamilika leo Kote nchini katika shule za msingi huku ikiwa imeashiria miaka 38 Katika mitihani ya KCPE.
Mwaka huu ndio ulikuwa mtihani wa mwisho wa mwaka wa enzi ambapo nchi inajiandaa kuhamia katika mfumo wa CBC ambayo imesifiwa kama mfumo unaolenga kuunda njia zaidi na wanafunzi na kupunguza shinikizo la kusaka alama za juu badala yake kujifunza ujuzi.
Ni wakati wa enzi hizi za KCPE ambapo nchi ilishuhudia kujitenga na siku za nyuma,huku serikali ikitangaza kuwa watahiniwa wote wataruhusiwa kukalia mitihani yao iwapo watakuwa wamejisajili au la.
Watahiniwa milioni 2.6 walisajiliwa kufanya mtihani huo wa KCPE na hukadiria asilimia 100 huku mtihani wa KPSEA ikichukuwa asilimia 40 ya mwisho ambapo asilimia 60 nyingine hutokana na mitihani endelevu ya darasani inayofanywa katika darasa la 4,5 na sita huku mitihani ya KPSEA ikiwa ni zaidi ya somo 6.