Waandaaji wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava Wamlipia Dudu Baya Faini ya Sh3 Milioni

Share this story

Waandaaji wa Tamasha la Miaka 30 ya Bongo Flava wamesema wamelipa faini waliyopewa pamoja na kumlipia msanii Godfrey Tumaini, maarufu Dudu Baya, faini ya shilingi milioni tatu iliyotolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Dudu Baya alitozwa faini hiyo na BASATA baada ya kubainika kuwa alikiuka mwongozo wa maadili ya sanaa wakati wa kutumbuiza katika tamasha hilo lililofanyika jijini Arusha.

Hatua hiyo ilikuwa miongoni mwa maamuzi yaliyotolewa na BASATA kufuatia tukio hilo, huku msanii huyo pia akizuiwa kushiriki shughuli za sanaa hadi atakapotekeleza masharti yaliyowekwa na baraza hilo.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post BASATA Yamtoza Dudu Baya Faini ya Sh3 Milioni
Next post Linda Mwananchi Yamtangaza Sifuna Kuwa Mgombea Urais wa 2027