Mgomo wa Sekta ya Usafiri Waendelea Kenya Kufuatia Kupanda kwa Bei ya Mafuta

Share this story

Mgomo wa sekta ya usafiri umeanza kushika kasi nchini Kenya huku waendeshaji wa magari ya umma, maboda boda, usafirishaji wa mizigo na sekta ya utalii wakipinga ongezeko la bei ya mafuta lililotangazwa hivi karibuni.

Mbali na huduma za uchukuzi wa umma, shughuli za usafirishaji wa mizigo, biashara na utalii zinatarajiwa kuathirika pakubwa kutokana na mgomo huo unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini. Shule nazo zinakabiliwa na changamoto za usafiri huku wazazi na wanafunzi wakihofia kucheleweshwa kwa masomo.

Kwa sasa, lita moja ya petroli jijini Nairobi inauzwa kwa shilingi 214.25 huku dizeli ikifikia shilingi 242.92, hali ambayo imeongeza mzigo mkubwa kwa wananchi na wafanyabiashara wanaotegemea mafuta katika shughuli zao za kila siku.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Ruto Heads to Azerbaijan to Market Kenya’s Affordable Housing Agenda at Global Urban Forum
Next post Tragedy as Rachel Wandeto Succumbs to Burn Injuries After Mwiki Attack