Malema Ahukumiwa Jela Miaka Mitano
Mwanasiasa wa upinzani nchini Afrika Kusini, Julius Malema, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kumiliki bunduki kinyume cha sheria na kufyatua risasi hadharani.
Mwaka 2018 Malema alinaswa kwenye video akifyatua risasi hewani wakati wa maadhimisho ya miaka mitano ya chama cha ‘Economic Freedom Fighters,’ ambapo amedai alikuwa anachangamsha wafuasi.