
NGOMA YA “GOD DESIGN” YA JUX YATIKISA TRENDING NO: 1 NIGERIA
Siku tano tu tangu atoe wimbo wake mpya God Design akiwa amemshirikisha rapa kutoka Nigeria, Phyno, msanii wa Tanzania Jux ameandika historia mpya katika muziki wa Afrika.
Wimbo huo, uliotayarishwa na Foxx Made It, umeweza kufikia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya video za muziki zinazotrend kwenye YouTube nchini Nigeria—ikiwa ni ishara tosha ya mapokezi chanya kutoka kwa mashabiki wa huko.
Kinachofanya mafanikio haya yawe ya kipekee zaidi ni jinsi tukio la harusi ya kifahari ya #JP2025 lilivyowagusa Wanaijeria, likizidi kuimarisha mapenzi yao kwa Jux, ambaye sasa si msanii tu bali pia anaonekana kama sehemu ya familia yao.