
Matasi Kutoshiriki Mpira Siku 90 Baadae Ya Kufungiwa Na FKF
Shirikisho la soka la nchini Kenya (FKF) limemsimamisha Golikipa namba moja wa Taifa hilo na Tusker FC Patrick Matasi kwa muda wa siku 90 kutokushiriki mashindano yoyote yanayoidhinishwa na FKF.
Hatua hii imechukuliwa kufuatia video zinazosambaa mitandaoni zikimwonyesha golikipa huyo akijadili juu ya upangaji wa matokeo katika mechi alizosimama langoni.
Shirikisho la soka nchini Kenya FKF linashirikiana na FIFA na CAF ili kufuatilia kwa kina suala hili.