
Benni McCarthy alaumu vifaa duni kama sababu ya kujiondoa CECAFA
Kocha mkuu wa Harambee Stars Benni McCarthy amezungumzia kujiondoa kwa Kenya kutoka kwa Mashindano ya Mataifa manne ya CECAFA, akitaja hali duni ya uchezaji na mazoezi ambayo anahofia inaweza kuhatarisha utayari wa timu hiyo kwa dimba lijalo la CHAN 2024.
Timu ya taifa tayari ilikuwa imesafiri hadi Karatu, Tanzania, na ilikuwa saa kadhaa kabla ya kuanza mechi yao ya ufunguzi wakati uamuzi wa kujiondoa ulipotolewa. McCarthy, ambaye alichukua jukumu kamili la uondoaji huo, alisema hali ya vifaa vilimwacha bila chaguo.
Kujiondoa kuliibua masikitiko kutoka kwa CECAFA, ambayo ilitoa taarifa kuelezea kujiondoa kwa Kenya dakika ya mwisho kuwa ya kusikitisha. Bodi ya eneo hilo ilishikilia kwamba wasiwasi uliotolewa na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) tayari ulikuwa umeshughulikiwa.