Vikundi vya bomeni vyafaidi hundi elfu kumi kujiinua ki uchumi.
Vikundi vya bomeni vyafaidi hundi elfu kumi kujiinua ki uchumi. Hii ni baada ya kiongozi wa Bomeni 2022 Mhesh Frank Mmare kuvikabidhi vikundi vya bomeni cheki za hundi la takribani elfu kumi kila kikundi ili kujiinua ki uchumi.
Katika sehemu ya kwanza ya zoezi hilo mheshimiwa Frank alisisitiza umuhimu wa jamii kuanzisha na kuziendeleza biashara ndogondogo ili kuto tumika vibaya na wanasiasa.
Project yake ya Haba na Haba community project ilivilete pamoja vikundi 15 kutoka kote bomeni,vikasaidiwa kusajili kisha baadae kupewa mafunzo(capacity building)na washikadau mbalimbali wakiwemo KCB,Equity,Qwettu Sacco,Uwezo Fund,Women Enterprise Fund na Ofisi ya Social Services na hatimae hii leo kutoa mchango wake wa start up.Hon Frank Mmare amevihimiza vikundi hivyo kuchukua mikopo mbalimbali kama vile Uwezo Fund , WEF na pia kujaza form za Bomeni ward grants kutoka kwa serikali ya county ili kujinufaisha zaidi.