Tottenham waanza mazungumzo rasmi kumsajili Savinho kutoka Manchester City
Klabu ya Tottenham Hotspur imeanza mazungumzo ya moja kwa moja na Manchester City kwa ajili ya kumsajili winga chipukizi Savinho. Vyanzo vinaeleza kuwa mazungumzo bado yanaendelea, huku mchezaji mwenyewe akionesha utayari wa kujiunga na Spurs iwapo pande zote mbili zitakubaliana ada ya uhamisho.
Kocha wa Tottenham, Thomas Frank, ameripotiwa kumtaja Savinho kama mchezaji anayekidhi vigezo vya kikosi chake kwa msimu ujao.
Chanzo: Fabrizio Romano