Thomas Frank ameachishwa kazi kama kocha mkuu wa Tottenham Hotspur.

Share this story

Tottenham Hotspur wamemwondoa Thomas Frank kazi kama head coach baada ya miezi 8 tu tangu aanze kuinoa Timu iyo.

Kulingana na ripoti, inasemekana Thomas Frank alikasirisha kikosi chake cha Tottenham Hotspur kwa kujadili mara kwa mara Arsenal kabla ya kutimuliwa kwake.

Meneja huyo wa zamani wa Brentford aliondolewa kwenye nafasi yake siku ya Jumatano, saa chache baada ya Spurs kupokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Newcastle United

Spurs kwa sasa wanakamata nafasi ya 16 kwenye msimamo na wanakabiliwa na hatari ya kutumbukia katika kinyang’anyiro kingine cha kushuka daraja baada ya kumaliza katika nafasi ya 17 msimu uliopita. Licha ya rekodi yao mbaya ya ndani, Spurs wamefuzu kwa raundi ya muondoano ya Ligi ya Mabingwa baada ya kuvuka awamu ya ligi wakiwa katika nafasi ya nne.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Eric Omondi Begins His Walk from Nairobi to Mombasa
Next post Pictures : Gov Wakujaa Joins Eric Omondi Charity Walk