Soko la zamani Mwatate na Wenyeji wa Kariobangi kufaidika na mradi wa kuinua hadhi ya mitaa ya mabanda
Wenyeji wa Kariobangi pamoja na soko ya zamani mjini Mwatate ambao wananuiwa kufaidika na mradi wa kuinua hadhi ya mitaa ya mabanda(Kenya informal settlement improvement project (KISIP 2) hii leo wameshiriki kikao na wataalam wa ardhi kutoka serikali kuu na Kaunti pamoja na mwanakandarasi GEODEV(K), agenda kuu ikiwa uhamasishaji kuhusu Mradi huo.
Walioshiriki wamepongeza juhudi za Gavana Andrew Mwadime Wakujaa, kwa kuimarisha uhusiano kati ya Kaunti serikali kuu na wadau wengine,jambo wanasema ni kiungo mhimu kwa maendeleo.
“Tunashukuru juhudi za Gavana Wakujaa na maono yake ya kuhakikisha maeneo yetu yamepangwa vyema.Mradi huu tunauunga mkono na tutashirikiana kuhakikisha umetekelezwa vilivyo.” Amesema Geoffrey Mwakina,mmoja wa wenyeji.
Serikali ya Wakujaa imelipa kipaombele swala la ardhi na umiliki,ili kuimarisha juhudi za kukuza uchumi.
Mradi huu utatumia Mwaka mmoja kukamilika.
Via The Taita Taveta County Government