Real Madrid Yapinga Vikali Mchezo wa LaLiga Kuchezwa Nje ya Hispania.

Share this story

Klabu ya Real Madrid CF imetoa tamko rasmi likieleza kupinga vikali pendekezo la kuchezwa kwa mchezo wa raundi ya 17 ya Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga) kati ya Villarreal CF na FC Barcelona nje ya mipaka ya Hispania.

Shirikisho la Uhispania liliidhinisha mpango wa La Liga kuitisha Barcelona dhidi ya Villarreal huko Miami, ambayo itakuwa mechi ya kwanza kabisa ya ligi kuu ya Ulaya huko Merika.

Katika taarifa hiyo, Real Madrid imesisitiza msimamo wake wa kutaka michezo ya mashindano ya kitaifa kuchezwa ndani ya ardhi ya Hispania, ikibainisha kuwa hatua ya kuhamishia mechi hiyo nje ya nchi inapingana na kanuni na historia ya mashindano hayo.

Klabu hiyo imeongeza kuwa inalinda maslahi ya mashabiki, wachezaji, na taswira ya soka la ndani.


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Govt Increase County Allocation Bill Into Law
Next post Boniface Kamau has been unveiled as the SportPesa Mega Jackpot millionaire