Raila Odinga afanya mkutano na Wazee wa Mombasa katika hall ya Sheikh Zayed
Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga anayegombania kiti cha uraidi kwa tikiti ya ODM leo amefanya mkutano wa wazee wa Mombasa katika hall ya Sheikh Zayed. Raila katika kampeni zake za mwaka ujao amekuwa akizungumzia kuhusu umoja na mkutano huu ni moja ya mikutano mingi aliyofanya ilikufanikisha Azima yake ya kuwa raisi kupitia muungano wa Azimio la Umoja.
Mkutano huo ulihudhuriwa na gavana wa Mombasa Ali Hassan joho na wabunge la eneo hilo.
Gavana Hali hassan Joho alirudisha shukrani zake kwa wazee waliojitokeza kwa mkutano huo.
Kupitia mtandao wa facebook aliandika
“Narudisha shukrani zangu za dhati kwa wazee wangu wa Mombasa. Katika Safari hii ya maendeleo mumekuwa nguzo muhimu na ya kuaminika. Basi tukamilishe hii safari kwa kusimama na Mhe. Raila Odinga mwakani 2022.”