Msanii wa muziki wa rap, Taymor Travon McIntyre ahukumiwa miaka 80 gerezani
Msanii wa muziki wa rap, Taymor Travon McIntyre maarufu kama TayK mwenye umri wa miaka 25, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo gerezani kwa kuhusika katika mauaji ya Mark Saldivar mwaka 2017, amepangiwa rasmi tarehe mpya ya kuachiliwa huru kuwa Agosti 8, 2099.
Tayk alipatikana na hatia kutokana na mchango wake katika tukio hilo la mauaji, ambalo lilisababisha kifo cha Saldivar, na amekuwa akihudumia kifungo cha muda mrefu. Tarehe mpya ya kuachiliwa imeibua mazungumzo mitandaoni kuhusu muda wa vifungo na athari zake kwa wasanii na mashabiki wao.