Mjumbe Wa Bandari FC Amjibu Ali Kamwe
Beki wa zamani wa Harambee Stars na mjumbe wa sasa wa bodi ya Bandari FC Ricky Solomon ametoa jibu kwa matamshi ya Ali Kamwe. Akizungumza katika mahojiano na Japhet Kahindi “Makanaky,” Solomon alisema kuwa Bandari wamejiandaa kikamilifu kwa changamoto hiyo na kuwaonya Yanga SC ya Tanzania kujizatiti ipasavyo. Aidha amefichua kuwa Coastal imeimarisha kikosi chake kwa kufanya usajili wa wachezaji wa kigeni wakiwemo wachezaji kutoka Cameroon na kutabiri kwa ujasiri kuwa Yanga itapoteza kwa goli 2 kwa 0.