Manchester United Kuingia Sokoni Januari Kusaka Mshambuliaji Wa Kumsaidia Rasmus Hojlund

Share this story

Manchester United wanapanga kuongeza mshambuliaji wa kumsaidia fowadi wao Rasmus Hojlund, mwezi Januari baada ya kuibuka wasiwasi juu ya maendeleo ya mchezaji huyo aliyepewa majukumu mazito akiwa na umri mdogo.

Hojlund tayari amefunga mabao matatu kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, ingawa anaonekana kuanza kwa kigugumizi kwenye Ligi Kuu England, baada ya kushindwa kupachika bao kwenye Ligi hiyo tangu awasili kutoka Atalanta.

Tayari United wameanza kuwafuatilia washambuliaji wenye uzoefu barani Ulaya ili kumpunguzia presha Hojlund, majina yanayotajwa zaidi ni mshambuliaji wa Brentford, Ivan Toney, ambaye pia anawindwa na klabu za Arsenal na Chelsea.

Vilevile mshambuliaji wa FC Porto Mehdi Taremi, mwenye miaka 31 ambaye amkuwa akihusishwa kuhamia Old Trafford msimu uliopita anaweza kuwa chaguo sahihi kwa United, wakati mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Iran ukiwa mbioni kutamatika mwisho wa msimu huu.

United pia imekuwa ikihusishwa kwa muda mrefu na mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen na huenda ukawa wakati sahihi wa Mashetani Wekundu kutupa karata yao ya ushindi ili kumsajili Fowadi huyo ambaye pia ni chaguo la timu mbalimbali barani Ulaya.

United wamefanikiwa kufunga mabao kumi na moja (11) kwenye Premier League, huku bao kutoka safu ya ushambuliaji likiwa ni moja kutoka kwa Marcus Rashford kwenye mechi dhidi ya Arsenal.

Ni wazi kuwa siku za, Antony Martial, zinahesabika ndani ya Old Trafford kwani mshambuliaji huyo amekuwa na wakati mgumu wa kufufua kiwango chake kufuatia majeraha ya mara kwa mara huku mkataba wake ukitamatika mwishoni mwa msimu huu.

Hivyo, katika juhudi za kulinda kibarua cha Kocha Erik Tan Hag, United wanapanga kuongeza nguvu kwenye safu ya Ushambuliaji mwezi Januari.

Aidha, United watarejea dimbani kutafuta pointi tatu pindi watakapo wavaa Fulham pale Craven Cottage mchana wa Jumamosi, ya Novemba 4.


Share this story
Previous post Mombasa Port to be concessioned to improve service delivery
Next post Mombasa Port to be concessioned to improve service delivery