Jacqueline Wolper, amethibitisha kuachana na Mume wake, Rich Mitindo

Share this story

Mwigizaji wa filamu na Mfanyabiashara nchini Jacqueline Wolper, amethibitisha kuachana na Mume wake, baba watoto wake Rich Mitindo, na kwa sasa anashughulikia suala la talaka.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper ameandika kuwa; “Hellow Mashabiki zangu, marafiki na Watanzania wote mnao nitakia mema.

Ni kwa masikitiko mengi sana mmekuwa mkinitumia message, links, na Clips mbalimbali, huku mkinishauri, kuniombea na kunitia moyo. Nimepokea msg zenu zote kwa moyo wa Shukrani sana. Na Mungu awabariki wote mnao nitakia mema, na hata wale wenye nia tofauti na njema pia mbarikiwe.

“Lakini naomba niwatoe wasiwasi na mashaka juu ya furaha na amani ya moyo wangu. Mimi na mzazi mwenzangu Rich (Baba P) hatupo pamoja (TUMEACHANA). Nipo kwenye process za Divorce/Talaka. Hivyo, mashauri yote na huruma juu ya mambo yanayo endelea na mzazi mwenzangu, msiyalete kwangu tena. Ni mtu ambae yupo huru kufanya chochote kinacho mpendeza.

“Na hii niseme tu si kwa ubaya haijalishi mtalipokeaje wengine lakini maisha halisi ya ndoa yangu nayajua mimi na mwenzangu kwahiyo tutabaki kuheshimiana kama wazazi na kulea watoto wetu lakini swala la mahusiano ya ndoa hilo halipo!

“Nawapenda sana nashukuru kwa msg zenu nyingi za kunitia moyo kutokana na mambo mnayoyaona huko lakini niwaambie tu mimi nipo sawa na muache kunihusisha na mambo yanayoendelea kwa mzazi mwenzangu kwasababu hayanihusu na nisingependa kuongelea hayo


Share this story

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Previous post Kindiki Tells Off Critics
Next post Abducted Social Media Influencers Peter Muteti and Billy Mwangi Released