ISAK ATANGAZA KUHITIMISHA SAFARI YAKE NEWCASTLE
Alexander Isak amethibitisha kuwa hatavaa tena jezi ya Newcastle United.
Hata kama dirisha la usajili litafungwa bila yeye kuondoka, nyota huyo wa Sweden anaona muda wake na klabu hiyo umefika mwisho na hatarajii kurejea tena kwenye kikosi.
Hata hivyo, Newcastle wamesisitiza kuwa hawana mpango wa kumuuza, ingawa wapo kwenye mchakato wa kutafuta mbadala wake sokoni.
Inadaiwa Isak alishaweka wazi tangu msimu uliopita kuwa ulikuwa wa mwisho kwake St James’ Park, na tayari amemwambia kocha Eddie Howe kuhusu nia yake ya kuondoka. Liverpool ilishatuma ofa ya pauni milioni 110 ikakataliwa, lakini Newcastle huenda ikakubali iwapo dau litakaribia pauni milioni 150.
Chanzo: David_Ornstein