Gavana Nassir ataka Mombasa Kusimama Nyuma ya Raila Kabla Ya Uchaguzi 2027
Gavana Abdulswamad Sherrif Nassir Jumatatu aliwaongoza viongozi wa Mombasa na wanachama wa ODM kutangaza kumuunga mkono Raila Odinga kama mgombea urais kwa Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Haya yanajiri huku Rais William Ruto akikamilisha ziara yake huko Nyanza ambayo wachanganuzi wengi wanaona kama jaribio la kumvuta Waziri Mkuu huyo wa zamani kwenye kona yake ya siasa.
“Ukitaka kuzungumza nasi, lazima ufanye hivyo kupitia Raila Odinga. Yeye ndiye kiongozi wetu na sisi kama uongozi wa kaunti ya Mombasa tuko nyuma yake kwa dhati,” Nassir alisema.